Menu
 


Na Shaban Kondo,

Shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya taifa ya Cameroon utakaochezwa katika tarehe ya FIFA ambayo February 6 jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa TFF Angetille Osiah amesema mchezo utatumika kama sehemu ya kujiandaa ya michezo ya kimataifa itakayoikabili Taifa Stars mwezi March, ambapo timu hiyo itacheza na timu ya taifa ya Morocco katika mpambano wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.

Hata hivyo kabla ya kupatikana kwa mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki, tayari shirikisho la soka nchini TFF lilikua limepokea maombi kutoka katika mataifa mbali mbali ya Afrika ambayo yalilenga kucheza na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

Kamati ya uchaguzi ya TFF hii leo imekutana kwa ajili ya kujadili mapingamizi yaliyowekwa na wadau wa soka nchini dhdi ya baadhi ya wagombea nafasi mbali mbali za uongozi wa shirikisho la soka nchini.

TUKIWA BADO KWENYE UCHAGUZI:- Kamati ya uchaguzi iliyo chini ya mwenyekiti Deogrtius Lyato ilianza mchakato wa kujadili mapingamizi kuanzia mishale ya saa nne asubuhi kwa kuwashirikisha wadau pamoja na wagombea waliolengwa.

Hata  hivyo mpaka muwakilishi wetua naondoka katika eneo la ofosi za shirikisho la soka nchini nchini alipata bahati ya kushuhudia pingamizi la Frank Mchaki dhidi ya mgombea nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu Mohamed Yahya pamoja na mgombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa bodi hiyo Said Mohamed likiwekwa kapuni kwa madai ya kukosa uthibitisho wa kutosha.

Hata Hivyo Frank Mchaki amesema hakuridhishwa na mwenendo wa pingamizi lake lilivyosikilizwa na kamati ya uchaguzi, kutokana na baadhi ya nyaraka kufanya kuwa siri.

Frank Mchaki alimuwekea pingamizi said Mohamed kwa madai ya kukosa sifa ya kuwani nafasi ya makamu mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu, kwa kigezo cha kukosa sifa ya kuwa mwenyekiti wa Azam FC, hatua mbayo imekua tofauti.

Mchaki pia alimuwekea pingamizi Mohamed Yahya kwa kigezo cha kukosa sifa ya kuwani nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu kwa kigezo cha klabu yake ya Kagera Sugar kushindwa kumaliza katika nafasi sita za mwanzo msimu uliopita, hivyo alidhani ameingia katika kinyang’anyiro hicho kupitia mtibwa sukari.

Hata hivyo ameshindwa kutetea pingamizi lake na kujikuta likiwekwa kapuni na kamati ya uchaguzi.

Post a Comment

 
Top