Menu
  

Na Ezekiel Kamanga,Mbeya
 Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Mbeya imewafikisha mahakamani watumishi wawili wa mahakama ya mwanzo Mwanjelwa kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kiasi cha shilingi elfu hamsini.Akisoma shitaka linalowakabili watuhumiwa hao mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Mbeya Zabibu Mpangule mwanasheria wa TAKUKURU, Joseph Muledya amesema watuhumiwa hao wametenda kosa hilo Januari 17 mwaka huu kinyume cha sheria kifungu namba 15 kidogo kwanza A cha adhabu ya mwaka 2007.Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Agnes Atanas Mitimingi mwenye umri wa miaka 33 karani wa mahakama hiyo na Majuto Simon Shombe ambaye ni askari mgambo katika mahakama hiyo.Aidha amesema watuhumiwa hao walimtaka Leonard Ngosha kutoa kiasi cha shilingi laki moja ili waweze kumsadia kushinda kesi inayomkabili lakini aliomba kupunguziwa na ndipo walipompunguzia hadi kufikia shilingi elfu themanini ambapo alitoa shilingi elfu hamsini kwa njia ya simu.Watuhumiwa wote wamekana shitaka linalowakabili na wapo nje kwa dhamana ya shilingi laki tano na kesi hiyo itasikilizwa tena Februari 4 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top