Menu
 Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha taarifa zinazodai kwamba akaunti ya shirikisho hilo imefungwa kufuatia sakata la mamlaka ya mapato nchini TRA kuishikilia kwa shinikizo la kutaka kulipwa fedha za makato ya kodi zilizostahili kulipwa kutokana na mishahara ya makocha wa timu za taifa kutoka nje ya nchi.


Katibu mkuu wa TFF Angetille Osiah amesema akaunti za TFF bado zinafanya kazi, na kilichofanywa na TRA ni shinikizo la kutaka fedha za makato ya kodi kulipwa hatua ambayo imeshafanyika.
 
Baada ya kukiri sehemu ya fedha zilizobaki kwenye akaunti ya TFF ilipelekwa kwenye vilabu vya ligi kuu kupitia kamati ya ligi, Angetille Osiah amesema wana uhakika sehemu ya fedha iliyochukuliwa na TRA itarejeshwa kwa wakati kufutia mazungumzo waliyoyafanya dhidi ya serikali pamoja na TRA
.

Angetille Osiah amesema suala hilo limefikia pazuri na tayari wameshawasiliana na kamati ya ligi kwa ajili ya kuvitaka vilabu kuheshimu taarifa iliyotolewa na serikali kwa ajili ya kurejeshwa kwa fedha zilizochukuliwa ambazo zitasaidia maandalizi kwa timu za ligi kuu ambazo zina deni la kumaliza mzunguuko wa pili unaotarajiwa kuwanza January 26.
Kama itakumbukwa vyema naibu waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo, Amos Makala alitoa uhakika kwa upande wa serikali ambapo alisema ligi kuu ya soka Tanzania bara itaanza kwa wakati kutokana na uhakika wa suala la upatikanaji wa fedha za vilabu kwa wakati.

Post a Comment

 
Top