Menu
 


Taifa Stars

Taifa Stars

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeanza mazoezi rasmi hii leo baada ya kuingia kambini January sita kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia utakaochezwa jijini Adis Ababa January 11.

Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Bonifas Wambura amesema kikosi cha Taifa Stars kimelazimika kuanza mazoezi rasmi hii leo na itafanya mafunzo asubuhi katika Uwanja wa Karume na jioni katika Uwanja wa Taifa.

Aidha amesema kuwa saa 9 alasiri timu hiyo ya taifa itaelekea Nchini Ethiopia kwa ajili ya mechi ya kirafiki na Januari 12, mwaka huu itarejea Dar es salaam na kwamba wachezaji wote wamesharipoti kambini isipokuwa wachezaji wawili wa  Yanga ambao wapo Uturuki. 


Katika hatua nyingine Bonifas Wambura ametoa ufafanuzi wa taratibu za mazungumzo zilizofanywa kati ya TFF dhidi ya viongozi wa klabu za  Simba, Dar es salaam Yong Africans, Azam FC pamoja na Matibwa Sukari ambazo ziliweka msimamo wa kutowatoa wachezaji wao katika kipindi hiki cha kujiandaa na mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka tanzani bara uliopangwa kuanza januari 26.
 
Kama itakumbukwa vyema uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa katibu mkuu Evodius Mtawala ulitangaza msimamow a kutokua tayari kuwaachia wachezaji wao kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa kwa kisingizo cha maandalizi ya mzunguuko wa pili na michuano ya kimataifa, lakini msimamo huo umekua tofauti na badala yake wamekubaliana na TFF kuwatoa wachezaji walioitwa na kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen.

Post a Comment

 
Top