Menu
 

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo akikata utepe kuzindua na kufungua ofisi ya waendesha bajaji mkoa wa Mbeya eneo la Isanga

Naibu waziri Mulugo akishangiliwa na wanachama wa chama cha waendesha bajaji mkoa wa Mbeya mara baada ya kuzindua ofisi yao

Katibu mkuu wa chama cha waendesha bajaji mkoa wa mbeya Ernest Mwaisango akisoma risala kwa mgeni rasmi...
Na Geophrey Kindimba,Mbeya.
Vijana mkoani Mbeya wamesema wamechoshwa na tabia ya baadhi ya wanasiasa kuwatumia kufanya vurugu badala ya kuwawezesha mbinu ya wao kujikwamua na tatizo la ajira.Wameyasema hayo leo kupitia risala iliyosomwa na katibu wa madereva wa bajaji mkoani Mbeya Ernest Mwaisango wakati wa sherehe ya kuzindua umoja wao ambapo mgeni rasmi wa sherehe hizo alikwua naibu waziri wa elimu Philipo Mulugo.Mwaisango amesema kwa kipindi cha miaka miwili sasa vijana weni wamekuwa wakishindwa kujituma kwenye shughuli za kujiingizia kipato utokana na kushawishiwa kuingia barabarani kufanya fujo na maandamano yasiyona tija kwao.Akijibu risala hiyo Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Mulugo amesema hiyo ni hatua muhimu kwa vijana kutambua nafasi zao katika kulitumikia Taifa ambapo amesema Serikali inawadhamini na kuwawezesha kwa haraka vijana ambao watakuwa wamejiunga katika kikundi kimoja na kusajiliwa.Aidha Mulugo ametoa msaada wa shilingi milioni moja na laki 9 kwa madereva wa bajaji na pikipiki ambapo shilingi laki nne zimetolewa kwa ajili ya kulipia pango la ofisi ya bajaji, shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwahamasisha wanakikundi kuchangishana fedha ili waweze kununua bajaji zao wenyewe na shilingi laki tano imetolewa kwa madereva wa pikipiki ili kuwawezesha nao kuandaa mchakato wa kujisajili.

Post a Comment

 
Top