Menu
 


Serena Williams katika pozi.
 Nchini Australia:

Wachezaji tenisi nyota Maria Sharapova kutoka nchini Urusi na Venus Williams kutoka nchini Marekani wanatarajia kukwaana katika mzunguko wa tatu wa michuano ya wazi ya Australia inayoendelea jijini Melbourne.


Venus anatarajia kutumia ushauri atakaopewa na dada yake Serena Jameca Williams ambaye amewahi kumshinda mara tisa Maria Sharapova anayeshika namba mbili kwa uboara duniani.


Serena Williams amesema yuko tayari kumsaidia dada yake ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha na baadae kuumwa ili aweze kushinda mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.


Serena Jameca Williams ambaye anapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la michuano ya Australian Open amesema utakuwa mchezo mkubwa na anadhani dada yake Venus ambaye hajashinda taji lolote tangu mwaka 2008 hana cha kupoteza katika mchezo huo.

Post a Comment

 
Top