Menu
 


Mbeya.
 Wadau mbalimbali walioahidi kutoa msaada kwa familia ya Daudi Mwangosi wamekumbushwa kutekeleza ahadi zao ili kuiwezesha familia hiyo kujimudu kimaisha.Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa.Amesema licha ya ahadi mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa hakuna ahadi hata moja ambayo imetekelezeka hadi sasa.Wakati huohuo amesema tume iliyoundwa kwa ajili ya uchunguzi wa kifo cha Daudi Mwangosi kilichotokea Septemba pili mwaka jana imemaliza kazi yake na kutoa mapendekezo kwa viongozi wa jeshi la polisi waliohusika katika oparesheni hiyo iliyopelekea kuuawa kwa Mwangosi waweze kuwajibika.Hata hivyo amesema umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini unatarajia kumuanzishi mradi wa ufugaji kuku wa kisasa mjane wa Mwangosi ili aweze kuilea vyema familia yake.

Post a Comment

 
Top