Menu
 


Na Fammy Chonko
Wamiliki wa maduka ya kuuza nyama ya Ng’ombe jijini Mbeya wameiomba Serikali kutoa vibali kwa wakristo kuchinja ng’ombe ili kuweka ushindani katika shughuli hiyo ambayo imeanza kuingia kwenye mvutano kutokana na dini moja kumilikisha kazi hiyo.Akiongea na Bomba Fm katibu wa wamiliki wa maduka hayo Issa Goliati hivi karibuni bei kuchinja ng’ombe mmoja imepanda kutoka shilingi mia mbili hadi kufikia shilingi elfu moja baada ya baraza la waislam Tanzania (BAKWATA) kupandisha bei hiyo.Amesema bei hiyo imekaa kibiashara zaidi ya huduma na kuongeza kuwa wao hawako tayari kulipa kiasi hicho cha shilingi elfu moja.Wakati huohuo wametoa lawama kwa Serikali kushindwa kuyaboresha machinjio hayo ambayo awali yalifunguliwa Serikali ili yaweze kutoa huduma za kimataifa.

Post a Comment

 
Top