Menu
 


Familia ya aliyewahi kuwa diwani wa kata ya Iyela jijini Mbeya marehemu Nkwenzulu Tweve wameingia katika mgogoro wa kugombania eneo la mazishi baada ya familia hiyo kufikwa na kifo cha Elizabeth Sanga kilichotokeaa January 6 mwaka huu.Kutokana na sakata hilo Jeshi la polisi mkoani Mbeya lililazimika kuingilia kati ili kuondoa utata uliopo kwa kuwataka wanandugu kukaa kikao na kuridhia marehemu kuzikwa kwenye makaburi hayo yaliyoandaliwa na Mzee Nkwenzulu.Akizungumza katika kikao cha usuluhishi kilichofanyika nyumbani Air Port dada wa marehemu Elizabeth Sanga,  Teresia Tweve  amesema kilichomkera kupita kiasi ni kutopewa taarifa za mazishi kama ndugu wa karibu na kwamba suala la kuzikwa marehemu ni popote hana kipingamizi chochote.Kwa upande wake balozi wa Mtaa wa Iyela two  Bubili Kajigili amemshukuru dada wa marehemu na wananchi kwa kutokata tama na kutoa ushirikiano wa kutosha katika mazishi kama ilivyokuwa kwenye mazishi ya mume wa Marehemu Elizabeth Sanga, marehemu Nkwenzulu.

Post a Comment

 
Top