Menu
 


Wananchi wa kijiji cha Iduya kata ya Utengule Usangu wilayani Mbarali wamevunja nyumba mbili mali ya Hamisi Mwaipopo na Agrey Mwaipopo wakiwatuhumu kuhusika na vitendo vya wizi.Wananchi hao wamesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuchoshwa na vitendo vyao vya wizi ambapo jamii ilikuwa na hofu ya kuibiwa na kupigwa na vijana hao.Naye diwani wa kata hiyo Juntwa Mwaliwaje ametoa wito kwa uongozi wa kijiji hicho kuzijenga nyumba hizo ambazo zimevunjwa na wananchi bila ya kuwa na uhakika kama watu hao wanahusika na vitendo vya wizi.Aidha ametoa wito kwa wananchi wa kijiji cha Iduya kuondokana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watoa taarifa polisi endapo watakwua na mashaka na mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya uhalifu.

Post a Comment

 
Top