Menu
 


Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti mkoani Mbeya akiwemo mlinzi wa Maliasili iliyopo eneo la Airport, Kata ya Iyela aliyekutwa ameuawa nje ya ofisi hiyo iliyo karibu na Ofisi za Mahakama ya Rufaa ya kazi.Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amesema tukio hilo limetoka usiku wa kuamkia Januari 22 mwaka huu, majira ya saa nane usiku ambapo mlinzi huyo aliyefahamika kwa jina moja la Jofrey mwenye umri wa miaka 25 amekutwa ameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.Aidha tukio la pili limetokea wilayani Mbarali mkoani Mbeya ambapo Tobias Mwampashi, mkazi wa Mkola, Kongolo Mswisi amekutwa amefariki dunia baada ya kunywa sumu kutokana na wivu wa kimapenzi, baada ya kutuhumiwa na mkewe Bi. Mary Mwamlima (33) ya kuwa alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine kijijini hapo.

Tukio hilo limetokea Januari 21 majira ya saa kumi jioni baada ya mkewe kuulizwa na mkewe juu ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine ndipo alipohamaki na kwenda ndani kisha akachukua sumu aina ya Ninja na kunywa  na alifariki muda mfupi baada ya tukio hilo.

Baada ya uchunguzi kukamilika mwili wa marehemu ulisafirishwa hadi kijiji cha Itale, Wilaya ya Ileje mkoani hapa kwa mazishi.


Tukio la mwisho limetokea maeneo ya mafiati kata ya Maanga ambapo ALLY MSOKE amekutwa amejinyonga chumbani kwake

Post a Comment

 
Top