Menu
 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, John Samwel Malechela wakati wa mahafali hayo ya 23 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bungo Kibaha(Picha na Maktaba ya Sufiani Mafoto Blog). 

Na mwandishi wetu,
 Waziri Mkuu mstaafu John Samwel Malechela amepinga maombi ya baadhi ya wadau wanaopendekezwa kutondolewa kwa viti maalumu bungeni kwa madai kuwa kauli hizo haziendani na malengo ya usawa wa utawala hapa nchini.Ametoa kauli hiyo mbele ya wandishi wa habari jijini Dar es salaam baada ya kuwasilisha maoni yake kwa tume ya marekebisho ya katiba ambayo jana ilikuwa ikipokea maoni kutoka kwa viongozi wastaafu serikalini.Aidha ametaka katiba mpya ijayo itambue mabunge mawili ambayo yatasaidiana katika kutekelezaji wa majukumu endapo bunge moja litatoa mapendekezo yatafanyiwa kazi tena katika bunge la pili ili kupata kitu sahihi zaidi kwa maslahi ya wananchiKwa upande wake mwenyekiti wa tume ya kurekebisha katiba Jaji Msitaafu Joseph Warioba amesema zoezi la kupotekea maoni linaendelea vizuri na kwamba mpaka sasa zaidi ya makundi 80 yameshatoa maoni yao.Zoezi la kupokea maoni ya katiba mpya kwa makundi maalumu linatarajiwa kufikia kilele mwishoni mwa mwezi huu ambapo watapata mapumziko mafupi kabla ya kuendelea kufanya uchambuzi na kuandaa rasmu ya kwanza ya katiba.

Post a Comment

 
Top