Menu
 

NA EZEKIEL KAMANGA  MBEYA 

Askari polisi wa kituo cha polisi mkwajuni mwenye namba  G.68 pc JAFARI KARUME MOHAMED mwenye umri wa miaka  30 amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Mwambani Mkwajuni wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Kwa mujibu wa Kaimu  Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Barakael Masaki  amesema  Askari huyo alijeruhiwa ubavu wake wa kulia kwa kurushiwa risasi  February 6  katika mapambano ya kurushiana risasi na majambazi katika eneo la MatundasI Wilayani Chunya  

 Aidha amesema majambazi  wanne wakiwa na silaha  idhaniwayo kuwa aina ya Smg walivamia kituo cha mafuta kilichopo kijiji cha Matundasi mali ya Samora Muyombe na kupora pesa taslimu shilingi milioni mbili na laki mbili  wakitumia gari lenye namba za usajili  T.227 BST Toyota Corola iliyokuwa ikiendeshwa na SHABAN MSULE
  
 Katika tukio hilo jambazi SHABAN MSULE aliuawa kwa kupigwa risasi na gari  lililotumika katika tukio hilo limekamatwa na maganda 9 ya risasi aina ya Smg na Sar na risasi 6 zimeokotwa eneo la tukio. 

Mwili wa marehemu Askari G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED umehifadhiwa hospitalini hapo  na msako mkali unaendelea chini ya uongozi wa Mkuu wa upelelezi Mkoani Mbeya ROBERT MAYALA Askari  polisi na wananchi ili kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa waliohusika na tukio hilo

Post a Comment

 
Top