Menu
 


Kiungo kutoka nchini Uingereza Frank Lampard amesema anafurahishwa na kiwango chake ambacho kimekua chachu ya kuiwezesha klabu ay Chelsea kuhitimisha suala la ushindi pale inapohitajika.


Frank Lampard, ambae ataondoka mwishoni mwa msimu huu kufuatia mkataba wake wa sasa kufikia kikomo wakati huo, amezungumzo furaha hiyo baada ya kuwa sehemu ya mafabnikio yaliyopatikana mwishoni mwa juma lililopita ya kuibanjua Wigan kwa idadi ya mabao manne kwa moja.


Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, amesema kujituma kwake na kumini bado ana uwezo wa kufanya makubwa zaidi ndio siri ya mafanikio aliyonayo kwa sasa hivyo anaamini bado mengi mazuri yanakuja kutoka kwake, licha ya majeraha kumuweka nje kwa kipindi kirefu mwanzoni mwa msimu huu.
Nae meneja wa muda wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez ameungana na Frank Lampard kwa kusema bado anaamini mazuri yanakuja kutoka kwa kiungo huyo ambae anajipigia upatu wa kuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.


Benitez amesema kiwango cha Lampard kimekua kikibadilika siku hadi siku, hivyo haamini kama kitarejea nyuma zaidi ya kusonge mbele kwa ajili ya kusaka mafanikio zaidi.

Post a Comment

 
Top