Menu
 

 
Kiungo wa klabu ya Manchester United, Shinji Kagawa ameitwa tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Japan kitakachocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Latvia utakaochezwa kati kati ya juma lijalo.
 Shinji Kagawa ameitwa kwenye kikosi cha Japan ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu mwishoni mwa mwaka jana ambapo ilishuhudiwa akiukosa mchezo wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Oman ambayo ilikubali kuchapwa mabao mawili kwa moja.

Kwa kipindi kirefu kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, alikua nje akiugulia maumivu ya nyama za paja kabla ya kurejea mwezi Disemba mwaka jana na kuonyesha kiwango wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Man city ambao walikubali kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Japan Alberto Zaccheroni amesema amekuwa akimfuatilia nyota huyo katika michezo kadhaa aliyocheza na hivyo ameshawishika kumuitwa kwenye kikosi chake baada ya kurejea katika kiwango chake cha kawaida.

Kiungo mshambuliaji wa klabu ay Cardiff City Craig Douglas Bellamy amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales ambacho kinakabiliwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Austria utakaochezwa kati kati ya juma lijalo mjini Swansea.
Craige Bellamy mwenye umri wa miaka 33, amerejeshwa kikosini baada ya kukosa michezo minne ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia lakini uwezo na kujituma kwake kumemfanya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales Chris Coleman kumtaja katika kikosi chake.
Kwa mara ya mwisho Craige Bellamy aliichezea timu ya taifa ya Wales mwezi August mwaka jana wakati wa mchezo dhidi ya  Bosnia-Herzegovina ambao walichomoza na ushidni wa mabao mawili kwa sifuri.

Chris Coleman amesema kumrejesha Bellamy kikosini pia kutaongeza nguvu kwa wachezaji chipukizi ambao wanataka kujifunza kupitia kwa goji huyo, hivyo ana matarajio makubwa kwa kiungo huyo kutimiza yale yaliyokusudiwa.

Mchezaji mwingine alierejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales ni kiungo wa klabu ya West Ham Utd Jack Collison ambae hakupata kuichezea timu ya taifa lake mwaka mmoja uliopita ambapo kwa mara ya mwisho alionekana wakati wa mchezo wa kumbu kumbu ya aliekua kocha wa timu ya taifa ya Wales Gary Speed ambae ni marehemu ambapo Wales walicheza dhidi ya timu ya taifa ya Costa Rica.

Post a Comment

 
Top