Menu
 


Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amesema nafasi ya kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger haipaswi kuhojiwa na wachezaji wa timu hiyo wanapaswa kuwajibika kwa matokeo mabaya.Matumaini ya Arsenal kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamekuwa finyu baada ya kukubali kipigo nyumbani cha mabao 3-1 kutoka kwa Bayern Munich ya Ujerumani.Jumamosi iliyopita Arsenal ilipata pigo lingine baada ya kubanduliwa katika Kombe la FA kwa kufungwa bao 1-0 na Blackburn Rovers.Wilshere amesema Wenger ameifundisha klabu hiyo kwa miaka 16 na amekuwa akifanya kazi nzuri hivyo hauwezi kuhoji kuhusu uwezo wake.Arsenal kwasasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza wakiwa nyuma ya Tottenham Hotspurs kwa alama nne hivyo wana kibarua kingine cha kuhakikisha wanamaliza katika nafasi nne za juu ili waweze kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Post a Comment

 
Top