Menu
 


 
Muinjilisti Nicholaus Luwoneko Kamwagila mwenye umri miaka 35 mkazi wa Mtoni Mtongani jijini  Dar es salaam anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutumia maneno ya kichochezi dhidi ya dini nyingine kuhubiri kanisani.
 
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani mbeya Diwani Athumani, amesema mchungaji huyo alikamatwa Januari 30 mwaka huu, katika eneo la Iyunga nje ya Kanisa la Moravian ushirika wa Iyunga jijini Mbeya

Kamanda amesema uchochezi huo haukuwafurahisha baadhi ya waumini ambapo walitoa taarifa  polisi  na mchungaji huyo amekamatwa akiwa na cd na vipeperushi ambavyo ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea

Aidha kamanda Athumani amewataka wananchi wote kuwachukia kutowakumbatia wachochezi wa madhehebu ya dini yoyote ili kujiepusha na madhara ambayo yamekuwa yakionekana katika baadhi ya maeneo nchini na duniani.

Hata hivyo ametoa pongezi kwa wote wanaoendelea kuthamini amani, usalama na utulivu hususani waumini waliotoa taarifa hiyo na kufanikisha kukamatwa muinjilisti huyo.

Post a Comment

 
Top