Menu
 


Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Jamhuri ya watu wa Czech pamoja na klabu ya Chelsea, Petr Cech ametangazwa kuwa mchezaji bora wa nchi hiyo kwa mwaka 2012.Kipa huyo ambae amekua tegemezi kubwa la kikosi cha Chelsea katika ligi ya nchini Uingereza pamoja na michuano ya kimataifa ameshinda tuzo hiyo baada ya kujizolea kura nyingi zilizopigwa na jopo la wachezaji, makocha, maofisa wa shirikisho la soka nchini humo pamoja na waandishi habari ambao walihusika katika mchakato wa kumsaka mchezaji bora wa mwaka 2012.Kabla ya kutangazwa kuwa mchezaji bora kwa mwaka 2012, Petr Cech mwenye umri wa mika 30 alikua anashindanishwa na beki wa klabu ya Werder Bremen ya nchini ujerumani Theodor Gebre Selassie ambae ameshika nafasi ya pili pamoja na kiungo wa klabu ya Humburg Sv ya nchini Ujerumani Petr Jiracek.Sifa zilizompa nafasi Petr Cech kujinyakulia tuzo ya mchezaji bora wa Jamuhuri ya Czech ni kuwa sehemu ya kikosi cha klabu ya Chelsea kilichotwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2012 na baadae aliisaidia timu ya taifa lake kufika katika hatua ya robo fainali kwenye fainali za mataifa ya barani Ulaya zilizofanyika kwa ushirikiano wa nchi za Poland na Ukraine.

Post a Comment

 
Top