Menu
 


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 07.02.2013.


WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.


MNAMO TAREHE 06.01.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SENGA – KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA . HAMISI S/O LINGSON MATOKA,MIAKA 40,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KITONGOJI CHA MING’ONGO KIJIJI CHA SENGA ALIKUTWA PORINI AKIWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA . 

MAREHEMU AMBAYE ALIKUTWA NA JERAHA KUBWA KICHWANI ALIKUWA  ANARUDI NYUMBANI KWAKE AKITOKEA MAKAO MAKUU YA KIJIJI CHA SENGA KWENYE MKUTANO WA KAWAIDA WA  MAENDELEO YA KIJIJI . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA NJIANI NA KUMPIGA HADI KUFA . 

CHANZO  KINACHUNGUZWA .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO  JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WATATUE MATATIZO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. 

AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI.


MNAMO TAREHE 06.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO ENEO LA SOWETO JIJI NA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1.FRANK S/O CHARLES @ BUDA ,MIAKA36,KYUSA,BIASHARA MKAZI WA BLOCK - Q NA 2.

 FURAHA S/O CHARLES,MIAKA 22,MSAFWA,MKULIMA MKAZI WA ILEMI  WAKIWA NA BHANGI KETE 357 SAWA NA KILO 1 NA GRAM  785 .  WATUHUMIWA NI MUUZAJI  NA WAVUTAJI WA BHANGI.

 TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Signed by
 
                                                       [  BARAKAEL MASAKI – SSP ]
                                  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
      

Post a Comment

 
Top