Menu
 

Na Ezekiel Kamanga, Gabriel Mbwille.
Watu watano wamefariki dunia kwa kupigwa na radi leo katika wilaya za Mbozi na Mbarali mkoani Mbeya baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi ya mara kwa mara.
Katika tukio hilo watu watatu wa familia moja akiwemo mama na watoto wake wawili wakazi kitongoji cha mpanda kati Kata ya Nyimbili wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi leo wakati mvua ikiendelea kunyeesha majira ya saa saba za mchana.
Waliofariki ni JERUMANA KUMI HALINGA mwenye umri wa miaka 35, DAVID HALINGA mwenye umri wa miaka 5, KUMI HALINGA mwenye umri wa miaka 3 na kumjeruhi mtoto wa miezi 9 ambaye amekimbizwa katika katika zahanati ya kata ya Nyimbili.
Tukio la pili limetokea katika kijiji cha Magurula kata ya Utengule Usangu ambapo KASIM SAGUTANGU amefariki dunia kwa kupigwa na radi baada ya kunyesha mvua kubwa Februari 3 mwaka huu majira ya saa nane za mchana
Matukio yote hayo yamethibitishwa na maafisa watendaji wa vijijini hivyo ambapo kwa tukio la Mbozi limethibitishwa na mtendaji wa kijiji LEMSI NZOWA.

Aidha tukio jingine limetokea katika kijiji cha Mbagala kata ya Ilembo ambapo mke wa mchungaji wa kanisa la Moravian ushirika wa Kesaria Mch.MAGANGA aliyefahamika kwa KOTANIDA PETRO AU MAMA ALFA amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akiwa shambani kwake.

Mganga mfawidhi wa Kituo cha afya cha Ilembo Dakta NELSON JOJI amekiri kupokea mwili huo na kusema kuwa uchunguzi umekamilika.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMANI amethibitisha kutokea kwa matukio hayo yote. 

Post a Comment

 
Top