Menu
 


RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter anaamini kuwa Brazil ina nguvu za kutosha kiuchumi kwa ajili ya kuandaa michuano ya kihistoria ya Kombe ya Dunia 2014.


Kauli hiyo ya Blatter mwenye umri wa miaka 77 ameitoa mara baada ya kufanya kikao na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Aldo Rebelo kuzungumzia maendeleo ya ujenzi wa viwanja na miundo mbinu mingine kwa ajili ya michuano hiyo.


Akihojiwa na mtandao wa shirikisho hilo Blatter amesema ana uhakika wa asilimia mia moja kwamba Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia watakuwa tayari kwa ajili michuano hiyo kwa wakati.


Mbali na kauli hiyo ya Blatter FIFA pia ilitangaza tarehe ya kufanyika sherehe za upangaji ratiba wa michuano hiyo ambayo itakuwa ni Desemba 6 mwaka huu katika hoteli ya Costa do Sauipe iliyopo katika jimbo la Bahia.

Post a Comment

 
Top