Menu
 


Shirikisho la Soka Duniani-FIFA linakusanya vielelezo ambavyo vinaweza kupelekea kuichukulia hatua Montenegro baada ya taarifa ya kuwepo kwa vurugu kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake kwa wachezaji wa Uingereza katika mchezo baina ya nchi hizo ambao walitoka sare ya bao 1-1.

Taarifa kutoka gazeti moja nchini Uingereza ilidai kuwa beki wa Uingereza Ashley Cole alitemewa mate wakati golikipa Joe Hart alikuwa akitupiwa vitu wakati wa mchezo huo uliochezwa jijini Podgorica.

Uchunguzi wa FIFA katika tukio hilo utaanzia kwenye ripoti ya mwamuzi Jonas Eriksson aliyechezesha mtanange huo.

Akihojiwa kuhusu tukio hilo Hart amekiri kurushiwa vitu mbalimbali ikiwemo tishu lakini amesema katika mechi kama hizo matukio kama hayo yamekuwa ya kawaida kwa mashabiki wa timu pinzani ili kujaribu kukuvunja moyo.

Post a Comment

 
Top