Menu
 


Halmashauri ya Jiji la Mbeya imewasilisha mapendekezo ya kubadilishwa na matumizi ya uwanja wa ndege wa zamani uliopo kata ya Iyela na kuwa stendi kuu ya mabasi na eneo la uwekezaji.

Akiwasilisha ombi hilo kwa kamati ya ushauri ya mkoa inayojumuisha viongozi wa kidini, wanasiasa, wakuu wa wilaya, wabunge na vyombo vya ulinzi, mkurugenzi wa jiji la Mbeya JUMA IDI amesema kubadilishwa kwa matumizi hayo kutaliwezesha jiji kupunguza msogamano wa magari kati kati ya mji.

Aidha amesema katika eneo hilo wanatarajia kujenga maduka makubwa ya vitu mbalimbali, hoteli na kujenga miundombinu mingine itakayopendezesha mji.

Hata hivyo ombi hilo halikuweza kupitishwa na linatarajiwa kupatiwa majibu katika vikao vijavyo vya mabaraza ya halmashauri.

Post a Comment

 
Top