Menu
 

Kocha Mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 23,  watakaoingia kambini mwishoni mwa juma hili kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya kupambana na timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wa kuwani kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.

Kim Poulsen metaja kikosi hicho huku akiamini huenda mambo yakawa mazuri katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Morocco, kufuatia matokeo safi yaliyopatika katika michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Zambia pamoja na Cameroon.

Kabla ya kutangaza kikosi cha wachezaji 23 Kim Poulsen aliweka wazi namna anavyoendelea kuwafuatilia wapinzani wa taifa Stars na amebaini wana sialaha kali za maangamizi hivyo hana budi kujipanga kisawa sawa.

Wachezaji walioitwa upande wa makipa ni: Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam).

Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Wakati huo huo kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen aesema alitamani kuwa na kambi ya muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo, lakini hana budi kuheshimu mipango na ratiba ya ligi kuu ya soka Tanzania bara pamoja na ushiriki wa timu ya azam kwenye michuano ya kombe la shirikisho la soka barani Afrika CAF.


Mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainaliza kombe la dunia kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Morocco utachezwa mwishoni mwa juma lijalo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Post a Comment

 
Top