Menu
 Nguli wa soka wa zamani nchini Ujerumani, Franz Beckenbauer amedai kuwa meneja mtarajiwa wa klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola atakuwa chini ya shinikizo kubwa kufikia mafanikio yaliyowekwa msimu huu na meneja wa sasa Jupp Heynckes.


Kocha huyo wa zamani wa Barcelona anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa Bayern Julai mosi mwaka huu lakini Heynckes ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu ametengeneza pengo kubwa katika mbio za ubingwa wa Bundesliga kitu ambacho kinamuogopesha Beckernbauer.


Bayern kwasasa inaongoza Bundesliga kwa tofauti ya alama 20 baada ya kupambana kutoka nyuma mara mbili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fortuna Duesseldorf Jumamosi iliyopita.


Klabu hiyo kama ikishinda mechi tatu za ligi zinazofuata itakuwa tayari wametawazwa mabingwa wapya wa Bundesliga hiyo ikiwa ni mara ya 23 kushinda taji hilo.


Nguli huyo anadai kuwa kila mtu anafikiri mambo yanaweza kubadilika kwa klabu hiyo wakati Guardiola atapoanza kufundisha hivyo kama timu itachukua ubingwa kwa tofauti ndogo ya alama kuliko msimu huu watu wanaweza kukosa imani naye.


Maneno ya nguli huyo yaliungwa mkono pia na rais wa Bayern Uli Hoeness ambaye amesema anafikiri timu hiyo itakuwa bingwa wa ligi msimu huu hivyo shinikizo kwa Guardiola na klabu litakuwa kubwa.

Post a Comment

 
Top