Menu
 

Na Shaban Kondo.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Pedro anaweza kukosa mechi mbili za klabu yake baada ya kuumia msuli wakati akiitumikia timu yake ya taifa katika mchezo wa kundi I dhidi ya Ufaransa.

Nyota huyo alitolewa nje katika dakika ya 76 Jumanne iliyopita baada ya kuifungia bao la mapema timu yake dhidi ya Ufaransa ambayo inanolewa na Didier Deschamps na kuipaisha timu hiyo kileleni mwa msimamo wa kundi lao.

Maumivu hayo ya msuli yanaweza kumfanya mchezaji huyo kukosa mechi ya Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga kati ya timu yake Barcelona dhidi ya Celta Vigo Jumamosi na mchezo mwingine dhidi ya Real Mallorca mwishoni mwa wiki ijayo.

Pamoja na maumivu hayo tayari ilishathibitishwa kuwa Pedro atakosa mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali dhidi ya Paris Saint-Germain wiki ijayo baada ya kupata kadi ya pili ya njano katika mchezo dhidi ya AC Milan.

Post a Comment

 
Top