Menu
 

Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014, dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars uliopangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Afisa habari wa TFF Bonifas Wambura amesema msafara wa timu hiyo utakaokuwa na watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es salaam majira ya saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.

Wachezaji walioko kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco kilicho chini Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.

Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.

Post a Comment

 
Top