Menu
 


Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amesema suala la walimu hao kukamatwa na kufikishwa Takukuru ni suala la ngazi nyingine hivyo hawatakiwi kulizungumzia. 
  Askari polisi wakifika katika shule ya sekondari Forest kutuliza maandamano yao


 Na Abdulshakur Rajab, Mbeya.
Wanafunzi wa shule za sekondari wametakiwa kuachana na tabia ya kufanya maandamano ambayo hayana msingi badala yake wafuate utaratibu ambao unaweza kutatua matatizo yanayowakabili

Hayo yamesema na afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda kufuatia wanafunzi wa shule ya Sekondari Forest ambao waligoma kuingia darasani licha ya kuwa na mitihani ya ndani na kupanga kufanya maandamano hadi ofisi ya elimu mkoa maandamano ambayo hayakufanikiwa kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi za kuyazima.

Miongoni wa sababu zilizopelekea wanafunzi hao ni baada ya kuachiwa huru baada ya kukamatwa na TAKUKURU walimu wawili wanaoshutumiwa kuomba na kupokea rushwa kwa wanafunzi wachewaji shuleni, ambapo kwa siku hukusanya hadi shilingi laki moja na nusu na kuwaadhibu wanafunzi wasiokuwa na fedha kwa kuwainamisha kichwa na kuchapwa viboko.

Aidha sababu nyingine wanafunzi hao wakishinikiza kuondolewa kwa mkuu wa shule hiyo Cecilia Kakela ambapo wamedai amekuwa akishindwa kuwajibika katika kazi zake.

Kaponda amesema  maandamano na migomo isiyokuwa ya msingi imekuwa ikiwamisha maendeleo ya elimu sanjari na kushuka kwa kiwango cha elimu hapa nchini pamoja na kujenga uadui baina yao na viongozi

Aidha amewataka viongozi wa shule na waalimu kushughulikia haraka matatizo yanayowakabili wanafunzi hao pamoja na kutoa mrejesho ifikapo leo mchana.

Post a Comment

 
Top