Menu
 

Na Shaban Kondo.
Vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Dar es salaam Young Africans, wameondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wao wa ligi dhidi ya polisi Morogoro utakaochezwa katika uwanja wa Jamuhuri.


Katibu mkuu wa klabu hiyo Lawrence Mwalusako amesema hali ya wachezaji waliondoka kuelekea mkoani morogoro ipo vizuri na wana hakika wataendelea kufanya vyema kwa lengo la kuusogelea ubingwa wa msimu huu.
Kikosi cha Dar es salaam Young Africans, kinakwenda kupambana na Polisi Morogoro huku kikichagizwa na mafanikio ya kutopoteza mchezo hata mmoja tangu mzunguko wa pili wa ligi ulipoanza mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa sasa kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha kutoka nchini Uholanzi Erne Brandt kinaongoza msimamo wa ligi kikiwa na pointi 48

Kocha mkuu wa Kagera Sugar Abdallah Kibaden ametoa siri ya ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya mabingwa watetezi Wekundu wa Msimbazi Simba hapo jana.

Kibaden amesema kujituma na kujitambua kwa wachezaji wake ndio kulikua silaha kubwa ya kuwamaliza vigogo hao wa soka ambao kwa sasa wanatapa tapa.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Ashanti Utd iliyorejea ligi kuu ya soka Tanzania bara, umesema katu hawatafungua milango kwa wachezaji walioichezea klabu hiyo miaka ya nyuma na kujiunga na klabu nyingine za hapa nchini na badala yake watatoa kipaumbele kwa wachezaji chipukizi.Raisi wa klabu hiyo Msafiri Mgoi amesema lengo kubwa la kutofikiria kuwasajili wachezaji waliopita klabuni hapo, ni kutaka kutoa mwanya kwa wachezaji wengine kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.
Wakati huo huo mwenyekiti wa Tawi la Yanga Kinondoni Thomas Mdeka amewatupia dongo wapinzani wao wa jadi Simba kwa kuwaambia hawana namna zaidi ya kujipanga upya na kuangalia namna ya kurejea kwenye kasi ya ushindani.


Mdeka ambae ni mwanachama na shabiki mkubwa wa klabu ya Yanga amesema hali ilipo ndani ya klabu ya Simba kwa sasa inasikitisha, ambapo hata hivyo akatumia usemi wa adui muombee njaa, kwa kuonyesha ni vipi walivyo tayari kutwaa ubingwa msimu huu.

Post a Comment

 
Top