Menu
 


Afisa Tarafa ya Kiwanja Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Shilla Sheyo anatuhumiwa na Wananchi wa  kijiji cha Sinjilili kwa kutafuna fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kioski cha Maji Shilingi laki nane na nusu zilizotokana na michango ya Wananchi na Mkuu wa Wilaya Deodatusi Kinawiro.

Tuhuma hizo zilitolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Sinjilili ulioitishwa na Mtendaji wa Kata ya Itewe, Ntundu Chapa wenye lengo la kupata taarifa za mapato na matumizi pamoja na mradi huo wa Maji.

Akijibu tuhuma zinazomkabili Afisa tarafa hiyo Shilla Sheyo amsema Shilingi Laki tano alipokea kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Shilingi Laki tatu alizipokea kutoka kwa mtendaji wa Kijiji hicho Aziza Mwambogo na Shilingi elfu 50 zilitolewa na msamaria mwema na kuongeza kuwa baada ya kupokea fedha hizo alizipeleka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.

Naye Diwani wa Kata ya Itewe Emmanuel Mwileky amewaahidi wananchi kulifuatilia suala hilo, hata hivyo taarifa yuliyonayo sasa inadai kuwa kamati iliyoundwa na diwani huyo imepata shilingi laki tatu huku wakiambiwa kuwa fedha nyingine ipo hazina.

Post a Comment

 
Top