Menu
 

Na Shaban Kondo.
Mke wa mkuu wa chuo kikuu huria mstaafu cha Tanzania Dr.John Samwel Malecela na mbunge wa same mheshimiwa Anne Kilango amewataka wake za viongozi na wanawake kwa ujumla kutumia vizuri chuo kikuu huria kujiendeleza kielimu kwani elimu ni mkombozi.



Amesema hayo katika sherehe za kumkaribisha mkuu wa chuo mpya wa chuo kikuu huria Dr. Asharose sherehe zilizizofanyika katika ukumbi wa Mwinyi Katika  makao makuu ya chuo kikuu huria Kinondoni na kuagwa kwa aliyekuwa mwanzilishi mkuu wa chuo kikuu huria Dr. John Samwel Malecela.



Pamoja na majukumu mengi waliyokuwa nayo wake za viongozi na wanawake kwa ujumla lakini ni bora wake hao kujitengea muda wa kujisomea ilikuongeza uelewa wao katika fani mbalimbali katika vyuo mbalimbali kikiwemo chuo kikuu huria.



Amesema ilikujisomea mwanamke anahitaji nia ya dhati pamoja na ujasili katika kufikia lengo lake ilipia kuweza kulea vizuri familia na kufanya maendeleo makubwa katika jamii kwa ujumla.



Mheshimiwa Kilango amesema yeye bada ya kuhitimu shahada yake ya kwanjza ya biashara amekuwa na uwezo mkubwa wa kuchangia hoja mbalimbali katika vikao vya bunge tofauti na ilivyokuwa awali.



Hatahivyo ameitaka serikali kuongeza vifaa vya kujisomea ikiwa ni pamoja na vitabu na nyenzo za kujisomea ilikumrahishia mwanawa kitanzania kufanikisha usomaji wake.



Dr. John Malecela amekuwa mkuu wa chuo kikuu huria kwa miaka 20 tangu anzishwa kwake hadi baada ya rais wa jamuhri ya muungano Dr. Jakaya Kikwete kumteua Dr.Asha Rose Migilo kuwa mkuu mpya wa chuo hicho.

Post a Comment

 
Top