Menu
 Meneja wa kundi maarufu la TipTop Connection Hamisi Shabani Talitale aka ‘Babu Tale’ amefunguka kuhusu historia ya maisha yake akieka wazi kuwa bila msanii Ray C yeye asingejukana.
 
Babu tale ambae alianza kama msanii wa vichekesho akiigiza sauti za watu maarufu amesema alikuwa na uwezo wa kuigiza sauti zaidi ya 100 licha ya kwamba concentration yake baadae ilianza kupotea taratibu 

Tale amebainisha kwamba mtu aliemtoa kwenye game ni Ray C ambae alikutanishwa nae na marehemu Kaka yake pamoja na Dj Mackay wa East Africa radio.
 
Tale amesema kuwa alianza kumsikia Ray C wakati alipokuwa akifanya kipindi cha Music Box East Africa Radio zamani kidogo wakati huo akisoma kidato cha pili.
 
“Nilikuwa naigiza ‘sauti ya kibabu’ kwenye kipindi cha Ray C kilichokuwa kinaitwa Music Box enzi hizo East Africa radio’ baadae Radio One nao wakanisikia wakasema kwanini huyu asifanye hii kwenye kipindi chetu cha watoto nikawa naendelea”. Tale told BK
 
Hata hivyo mkali huyo ambaye amezaliwa December 31, mwaka 1982 amesema aliweza kufahamiana na Madee walipokutana Morogoro kwenye show wakati huo msanii wa kizazi kipya Madee anatamba na nyimbo yake inayoitwa “Mungu wasemehe masela” ambayo alifanya na TID.
 
“Baada ya kaka yangu kufariki,mwaka mmoja baadae nikafiwa na sister. Wakati huo Madee alinipa wazo kuwa tufanye wimbo mmoja unaeza uka hit. Nakumbuka Madee aliandika ile ‘kazi yake mola’ tukiwa kwenye Kenta tunaenda kwenye mazishi” Said Tale
 
Babu Tale ameeleza kwamba baada ya kutoka Morogoro walipofika Dar mtu aliewasaidia kuwakutanisha na P Funk ni Dj Mackay ambapo walimkabidhi mkwanja na Mackay akaenda kumlipa Majani.
 
Hata hivyo tale aliendelea kusema kwamba wakati madee alipokwenda kuweka sauti studio siku hiyo aliwakuta Mandojo na Domokaya wakifanya rehasle ya wimbo wao wa nikupe nini na ndipo wakamfanya chorus ya wimbo wa kazi yake mola.
 
Kila Madee alipokuwa akifanya nyimbo zake alikuwa anarusha TipTop kwa hivyo wakafanya kuwa kama kundi na baadae wakajiunga wasanii wengine kama MB Dog na Chelea man baadae wasanii wengine kama Keysha, Z Anto, Pingu, Kassim wakaongezeka licha ya kuwa waliobaki sasa hivi ni Tunda man, Madee, Deso na kuna kichwa kingine kipya ambacho hakijatambulishwa rasmi.


CHANZO : BAABKUBWA

Post a Comment

 
Top