Menu
 

Na Ezekiel Kamanga, Kyela

KATIKA  hali isiyokuwa  ya kawaida iliyowashangaza wengi ni baada ya babu aliyefahamika kwa jina la Edward  Mwakalebela (86) ambaye ni mganga wa tiba za jadi mkazi  wa kijiji cha Ndwanga  kata ya Katumbasongwe wilayani Kyela Mkoani Mbeya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 6 Anjela kifoji,


Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Sioni Ijuni  aliiambia Tanzania Daima kuwa ilikuwa saa 8 usiku wa kuamkia j,mosi  mtoto wake alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo ambapo aliamua kumpa huduma ya kwanza kwa kumkanda na maji ya moto na ndipo alipoona damu zikitoka sehemu za siri,


Alisema alipomhoji zaidi ndipo mtoto huyo alipomtaja babu huyo kuwa alimuingilia kimwili na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama na kuwa mzee huyo ambaye ni jirani yao alikuwa na mazoea ya kumtuma mtoto kana kwamba ni mjukuu wake kumbe alikuwa anatengeneza mazingira ya kumfanyia unyama huo,


Kutokana na hali hiyo mama huyo alidai kuwa aliamua kupeleka taarifa hiyo kwa mwenyekiti wa kijiji akiwa na mumewe Kifoji  Mwabusila waliye tengana naye ambaye wanaishi  jirani,ambapo mwenyekiti baada ya kuandika maelezo aliwaamuru waende polisi ili wapatiwe kibali cha kwenda kutibiwa hospitalini na wao kufanya hivyo,na polisi walimkamata mtuhumiwa na kumtia hatiani,


‘’Tulipokuwa kwa mwenyekiti wa kijiji babu huyo alikili kutenda kosa hilo na aliomba msamaha akidai ni shetani tu alimpitia huku akiomba mambo hayo wamalizwe kimya kimya bila kwenda polisi jambo ambalo lilikuwa gumu wao kulikubali na ndipo  taarifa ilipo pelekwa polisi ambao walikuja kumkamata’’alisema mama mzazi wa mtoto huyo,


Mwenyekiti  wa kijiji  hicho Dickson Mwakasinga alikili kuwepo na tukio hilo na kuwa baada ya kuletewa taarifa ya uwepo wa tukio hilo alifuata taratibu zote  na kumkabidhi  mtuhumiwa huyo mikononi  mwa polisi wilaya kwa hatua zaidi za kisheria,


Mganga  wa  zamu aliyemtibu mtoto huyo Tabu Mwakalundwa alikili  kumpokea mgonjwa huyo na kudai kuwa mtoto huyo aliingiliwa na kuharibiwa vibaya na wao wanafanya jitihada za haraka za kumtibu mtoto huyo ili arudi katika hali yake ya kawaida,


Wananchi  wa kijij hicho kwa upande wao wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwa kuwa mzee huyo ni mganga wa tiba za kienyeji(asili) na kuwa umri alionao na kitendo alicho mfanyia mtoto huyo wa umri wa miaka 6 ni kinyume na maadili ya mtanzania,

Post a Comment

 
Top