Menu
 

Muda huu jeshi la polisi limevamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha Mh.Godbless Lema kinyume cha Sheria.


Kamanda Lema amewataka jeshi la polisi kufuata sheria kwani Sheria hairuhusu polisi kuingia kwenye makazi ya watu kuanzia saa 12 jioni hadi saa 12 asubuhi isipokua kama kuna kibali maalumu (Special warranty) ama kwa amri maalumu na halali kisheria ya mahakama.

Amewazuia kuingia nyumbani kwake lakini wametumia nguvu kuingia nyumbani kwake.

***DR.Slaa na IGP***

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa amemaliza mazungumzo yake na mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema muda huu.IGP amemuahidi Dr.Slaa kwamba ataongea na kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha kuhusiana na suala hili ambalo linafanyika kinyume cha sheria

Nitaendelea kuwaletea updates .....

- Ben Saanane- JF.

Post a Comment

 
Top