Menu
 

Chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini wamekutana na wandishi wa habari kuzungumzia moja wapo ya wito alioutoa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Kikwete kuvitaka vyombo vya habari kuimarisha amani  ya nchi.Wakizungumza katika Mkutano huo baadhi ya waandishi wa habari walioshirikia katika mkutano huo wamesema mojawapo ya mambo yanayochangia kuvurugika kwa amani nchini ni pamoja na baadhi ya wanasiasa kuvitumia vyombo vya habari kwa maslahi yao binafsi.Katika mkutano huo Tumaini Mwailage na mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari Mkoa wa Dar es salaam Jane Mihanje wamesema katika kuhakikisha amani inaimarishwa nchini vyombo vya habari vinatakiwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari kuwalipa vizuri wafanyakazi wao.Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini MOAT Reginald Mengi amesema ni vizuri kama wanahabari wakatoa mapendekezo ya namna ambavyo amani ya nchi inaweza kulindwa.

Post a Comment

 
Top