Menu
 

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeamua kuimarisha ufuatiliaji wa viwanja vinavyoandaliwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho nchini Brazil baada ya waandaaji kushindwa kumaliza kwa wakati uwanja wa ufunguzi wa michuano hiyo uliopo jijini Brasilia.FIFA pia imesisitiza Jumanne kuwa ucheleweshwaji wa namna hiyo hautavuliwa kwa viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe Dunia 2014.Baada ya kuchelewa kwa ufunguzi wa uwanja Brasilia na ikiwa imebakia miezi kama miwili kabla ya michuano ya Kombe la Shirikisho, FIFA ilikutana na kamati ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2014 na kutangaza kuwa wataanza ukaguzi upya ndani ya wiki mbili zijazo.Uwanja wa Taifa uliopo katika mji mkuu wan chi hiyo ulitakiwa kufungiliwa Jumapili iliyopita lakini kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kushindwa kwa zoezi la upandaji nyasi ilibidi waandaaji wasogeze mbele mpaka Mei 18 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top