Menu
 

 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro akizungumzana waandishi wa habari ofisini kwake

 Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka viongozi wa dini kutoa ushauri kwa waumini pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya mauji ya kikatili vivavyo endelea kujitokeza siku hadi siku katika maeneo yote Mkoani hapa yanayo hatarisha uvunjifu wa amani na kuliletea sifa mbaya jiji la Mbeya,

Kandoro aliyasema hayo jana  wakati wa sherehe za maadhimisho  ya sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo kimkoa yalifanyika Wilayani Rungwe na kuhudhuria na viongozi mbalimbali kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa Mbeya,baada ya kutokea matukio mfululizo ya mauaji ya kinyama yanayohusishwa na imani za kishirikina,

Baada ya kutoa ushauri huo kwa viongozi wa dini,Mh,Kandoro pia alizungumzia mfumo wa serikali mbili Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo yenye dola inayo shughulikia  Utawala,Ulinzi na usalama na masuala yote ya muungano na mambo ya Tanzania Bara yasiyo ya muungano,

Alisema kuwa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina mamlaka juu ya mambo yasiyo ya muungano yanayohusu Zanzibar  tu kama ilivyoainishwa katika sehemu ya kwanza ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake,

Aliongeza kuwa Kila mmoja wetu anao wajibu wa kudumisha umoja,mshikamano na muungano wetu kwa kuwaenzi waasisi wa Muungano wetu ambao ni Hayati Baba wa Taifa Mwl ,Julius Nyerere pamoja na Hayati  Sheikh Abed  Karume ambao walipiga vita udini,ukabila, Rushwa na aina zote za ukiukwaji wa haki za binadamu,

‘’Ndugu zangu wana Rungwe na wana Mbeya wote tunatakiwa tuuenzi Muungano wetu pamoja na kudumisha Amani,Utulivu,Upendo na mshikamano  miungoni mwa watanzania na majirani zetu,kupiga vita umasikini,ujinga na maradhi, kuimarisha misingi ya Utawara bora na Demokrasia’’,alisema Kandoro,

Aidha Kanoro aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kupambana kikamilifu na maambukizi  mapya ya UKIMWI,kupinga  vitendo vya Rushwa,na  imani za Kishirikina zinazopelekea mauaji ya wananchi wasio na hatia,na kuwataka kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kunufaika na huduma bora za Afya kwa kuchangia fedha mara moja tu kwa mwaka,

Pia  ailiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuri  mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,nyumba za waalimu pamoja na ununuzi wa madawati ili kupunguza changamoto katika shule zetu na vijana wetu waliopo katika shule za msingi na sekondari waweze kusoma vizuri  na kupata matokeo mazuri pindi wamalizapo masomo yao.

Post a Comment

 
Top