Menu
 

Nahodha wa timu ya taifa Tanzania Taifa stars Juma Kaseja ama Juma  Juma amewataka Watanzania kuendelea kuonyesha ushirikiano na timu ya taifa kwa ajili ya kuiwezesha kufanya  vyema kwenye michuano ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.

Mbali na mashabiki wa soka nchini, pia Kaseja amewataka viongozi wa serikali kushikamana na wadau wengine kwa hali na mali kwa ajili ya kuhakikisha dhana ya mafanikio inatimia kwa timu hiyo.

Katika hatu nyingine Afisa wa Wizara ya  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Charles Yesse Matoke ameungana na kipa huyo wa klabu ya Simba katika harakati za kuhimiza umoja ambao ndio siri ya mafanikio.

Matoke amesema kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha kwa watanzania wote dhidi ya timu yao ya taifa, kutakua na hitaji kubwa la wachezaji kusaka ushindi wanapokua katika uwanja wa nyumbani na ugenini.

Kama itakumbukwa vyema, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara alitangaza kamati ya Ushindi ya Taifa Stars ambayo itafanya kazi na wadau wwa michezo kwa ajili ya kuhakikisha timu ya taifa inafanya vyema kwenye michezo ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ukanda wa barani Afrika.

Kuundwa kwa kamati hiyo kumeonyesha wito wa nahodha Juma Kaseja kuitikiwa vyema na serikali ya awamu ya nne ambayo inaongozwa na Raisi Jakaya Kikwete ambae ni mdau wa kwanza nchini kwa sasa anaependa michezo.

Kamati iliyoundwa na waziri wa habari utamaduni na michezo hapo jana inaongozwa na Mohamed Dewji kwa kushirikiana na Teddy Mapunda (Montage),  Dkt. Ramadhani Dau (Mkurugenzi Mtendaji NSSF), Dioniz Malinzi (Mwenyekiti BMT), Abji Shabir (New Africa Hotel) pamoja na George Kavishe (TBL).

Wengine ni Mohamed Raza (Zanzibar), Leodger Chilla Tenga ( Raisi TFF), Joseph Kusaga (Clouds Media Group), John Komba (Mbunge) pamoja na Zitto Kabwe (Mbunge).

Post a Comment

 
Top