Menu
 

Kiungo kutoka nchini Ufaransa Samir Nasri ameustajaabisha ulimwengu, pale alipokiri kumkumbuka aliekua meneja wake wakatio akiitumikia klabu ay Arsenal Arsene wenger baada ya kukabiliwa na matatizo ndani ya kikosi cha Man City anachokitumikia kwa sasa.

Samir Nasri amesema tangu aanze kucheza soka, hakuwahi kufanya kazi kwa wema na mapenzi kama ilivyokua kwa Arsene Wenger, ambae alimsajili mwaka 2008 akitokea kwenye klabu ya Olympique de Marseille kwa ada ya uhamisho wa paundi million 12.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, imemlazimu kukumbushia maisha yake akiwa ndani ya klabu ya Arsenal chini ya utawala wa Arsene Wenger, baada ya kuweka wazi bifu lake na meneja wa klabu ya Man city ambae alitoa maneno makali dhidi yake mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Newcastle Utd ambao walikubali kichapo cha mabao manne kwa sifuri.

 Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo, meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini alimzungumzia Samir Nasri kwa kumkejeli ambapo alisema tangu alipomsajili kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 24 akitokea Arsenal, hakuwahi kucheza vyema kama ilivyokua katika mchezo dhidi ya Newcastle Utd.

Mancini pia kasema siku zote alikua akimuelekeza kucheza vyema kiungo huyo, lakini amekua mgumu wa kuelewa hatua ambayo imekua ikimpa msukumo wa kutamani kumchapa vibao ama kumbamiza manguni.

Kauli hiyo imeonyesha kumkera Samir Nasri na kuthibitisha wazi kwamba meneja huyo amekua na chuki nae kwa siku nyingi na pia amemtaka kutosita kumpiga pale atakapojisikia endapo atajiona ana mamlaka hayo.

Kufuatia utata huo Samir Nasri amekiri kumkumbuka Arsene Wenger kwa huduma nzuri ya ufundishaji anayowapa wachezaji wake na kuamini hakuwahi kufanya kazi vyema na meneja yoyote duniani zaidi ya babu huyo wa kifaransa.

Kutokana na hali hiyo tayari wadadisi wa soka duniani wameanza kuhisi safari ya Samir Nasri kuendelea kuwepo Man City ikawa imeishia msimu huu, kutokana na hatua ya kuweka wazi ugomvi wake dhidi ya Roberto Mancini.

Samir Nasri amekua na wakati mgumu ndani ya Man City msimu huu ambapo imeshuhudiwa akifunga mara moja katika michezo 21 aliyocheza.

Post a Comment

 
Top