Menu
 

Na Shaban Kondo,,,,
Taarifa za kupigwa kwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamuhuri Kiwelu Julio mara baada ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza dhidi ya Toto Africans, bado hazijawasilishwa kwenye ofisi za shirikisho la soka nchini TFF.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema endapo tukio hilo lilitokea na kushuhudiwa na muamuzi aliechezesha mchezo huo, huenda likawa limeoriodheshwa kwenye taarifa itakayowasilishwa kwenye ofisi za shirikisho hilo wakati wowote kuanzia sasa.

Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Toto African, John Tegete amekana madai ya wachezaji wake kuhusishwa na sakata la kupigwa kwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamuhuri Kiwelu Julio mara baada ya mchezo wa ligi mwishoni mwa juma lililopita.

John Tegete ambaye ni baba mzazi wa mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete amesema wachezaji wake hawakuhusika kabisa na tukio hilo, na ukweli ni kwamba Jamuhuri Kiwelu Julio alipigwa ngumi ya jicho na shabiki wa Toto Africans ambae aliokua pembezoni mwa gari la timu hiyo.

Chanzo cha kocha huyo kupigwa kinadaiwa kuwa alikwenda kwenye gari la Toto Africans mara baada ya mchezo kumalizika na kuchomoa ufunguo wa gari hilo kwa madai kulikua na mpira ambao alihitaji urudishwe.

Hata hivyo pamoja na Julio kuendelea na utaratibu wa kutaka mpira urudishwe alihakikishiwa na viongozi wa klabu ya Toto kuwa mpira haukuwepo ndani ya gari la timu hiyo na ndipo zahma ya kupigwa ilipojitokeza.Sakata la baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba wanaoutaka uongozi wa klabu hiyo ulio chini ya Ismail Aden Rage kujiuzulu linaendelea, kwa wanachama hao kubisha hodi katika ofisi za msajili wa vilabu na vyama vya michezo nchini.

Mmoja wa wanachama hao ambae pia ni mwenyekirti wa tawi la mpira Pesa Ustadh Masoud amesema wameamua kwenda kwenye ofisi za msajili kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko yao ya kusiginwa kwa katiba ya Simba ambayo wamedai haitendewi haki na mwenyekiti aliopo madarakani pamoja na jopo lake la uongozi.

Mbali na maelezo hayo ya kubisha hodi katika ofisi za msajili, Ustadh Masoud akamkumbusha mwenyekitiw a klabu ya Simba Ismail Aden Rage kwa kumueleza kwamba kwa sasa anawaongoza wanachama wanaoifahamu katiba yao ipasavyo hivyo amemtaka kuacha fikra za kizamani za kuamini anawaongoza watu wasiokuwa na ufahamu wa katiba yao.

Post a Comment

 
Top