Menu
 

Raisi wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga amekabidhi santuri ya mpango wa maendeleo ya soka, kwa lengo la kusaidia ukuzaji na kulea vipaji vya soka kwa vijana kwa wadau wa michezo nchini ambao waliongozwa na katibu mkuu wa baraza la michezo taifa Henry Lihaya.


Katika hafla hiyo Tenga amesema santuri hiyo anaamini itasaidia mpango wa kukuza soka nchini kwa kuwashirikisha viongozi wa serikali pamoja na wadau wa michezo ambao kila siku wamekua na hamu ya kuiona Tanzania inasonga mbele katika sekta hiyo.


Hata hivyo mpango huo umeonyesha kupokelewa vyema na baraza la michezo la taifa BMT kupitia kwa katibu mkuu wake Henry Lihaya, ambapo amesisitiza kuendelezwa kwa mikakati ya usaidizi wa kulea na kukuza vipaji kwa vijana ambao ndio watetezi wa taifa la Tanzania siku za usoni.


Lihaya pia akawataka viongozi wa vyama vingine vya michezo kuiga mfumo wa TFF wa kutengeneza njia kwa vijana ili kuiuwezesha Tanzania kuwa na dira nzuri ya michezo.

Post a Comment

 
Top