Menu
 

Ujumbe wa shirikisho la soka duniani FIFA umamaliza shughuli ya kuisikiliza malalamiko ya baadhi ya waliokua wagombea wa nafasi za uongozi wa shirikisho la soka nchini ambao waliondolewa na kamati ya uchaguzi pamojana kamati ya uchaguzi ya rufaa.

Ujumbe huo ambao ulikuwa chini ya mkuu wa idara ya wanachama wa FIFA Primo Cavaro hii leo jioni umekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia kwa kina suala hilo ambalo litawasilishwa kwenye makao makuu ya FIFA na kisha majibu yatarudishwa baada ya siku saba zijazo.

Primo Cavaro amesema suala walilokuja kulifanya hapa nchini ni kubwa hivyo yeye pamoja na timu yake hawawezi kutoa majibu ya moja kwa moja.

Post a Comment

 
Top