Menu
 


Mwanariadha nyota wa mbio fupi Usain Bolt ameshindwa kufikia rekodi yake ya dunia aliyoweka katika mbio za mita 150 wakati alipofungua msimu kwa ushindi kwenye mashindano yaliyofanyika kwenye ufukwe wa Copacabana jijini Rio de Janeiro, Brazil.

Bolt ambaye ni bingwa mara sita wa medali za dhahabu katika michuano ya olimpiki alishinda mbio hizo kwa kutumia muda wa sekunde 14.42 lakini alishindwa kuifikia rekodi yake aliyoweka mwaka 2009 jijini Manchester, Uingereza ya sekunde 14.41.

Akihojiwa mara baada ya mashindano hayo Bolt amesema hayo ni mashindano yake ya kwanza na anashukuru kuanza msimu mpya vyema huku akisubiri kwa hamu mchuano ya olimpiki 2016 itakayofanyika katika jiji hilo.

Katika mashindano hayo Bruno Lins wa Brazil alishika nafasi ya pili kwa kutumia sekunde 14.91 akifuatiwa na Alex Quinones wa Ecuador na Daniel Bailey wa Antigua na Barbuda waliomaliza katika nafasi ya tatu na nne.

Post a Comment

 
Top