Menu
 

Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards zinahusisha nyimbo, wasanii na watengeneza muziki waliofanya vizuri kuanzia Januari hadi Disemba kwa mwaka husika. Kufanya vizuri inahusisha kazi kuwa nafasi za juu katika chati mbalimbali za vituo vya redio au TV nchini na kukubalika kwa wengi mwaka uliopita. 

Nyimbo zilizotolewa mwezi Disemba hutokea kutoingia katika tuzo kutokana na kutofikia vigezo vilivyotajwa hapo juu kwa kutofanya vizuri katika MWAKA HUSIKA na huwekwa katika mwaka unaofuatia (mfano: wimbo wa Kamiligado wa Profesa Jay uliotoka Disemba 2011 na kuwekwa mwaka 2012) na mfano mwaka huu wimbo wa 2030 wa ROMA uliotoka mwezi Disemba 2012 na kufanya vizuri mwaka 2013 hivyo una nafasi mwaka ujao. 

Uteuzi hufanywa na Academy maalum inayohusisha wadau zaidi ya 50 toka vituo mbalimbali vya redio/TV, kumbi za muziki nk kote nchini ambao huketi na kupitia nyimbo zote na kuchagua zilizokidhi vigezo na kuziweka katika vipengele husika kisha kupiga kura kwa njia ya kielektroniki mpaka zinapopatikana tano zilizokamata nafasi ya juu.

 Utaratibu wa namna zoezi la upigaji kura kwa washindani wa mwaka huu utatolewa wiki hii.

 Like · ·
  • Fadhili Mbogolo and 88 others like this.
  • Michael Minja Tupo pamoja ila naomba zoezi hili liwe la haki isje ikawa mtu kapigiwa kura nyingi kisha hapewi tuzo na badala yake anapewa mtu mwingine nini maana ya kuwa na majaji sasa wakati wananchi ndio wanaoweza kuwachagua. Hivyo zoezi liendeshwe vizuri ili kuep...See More
  • Greyson Chris Bee Salufu Sina Ushabiki na Tunzo za T.H.T..... Tunzo uchwara za KILLI TANZANIA MUSIC AWARDS... Jipangeniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Hata niwe na Wivu kiasi gani siwezi kuonea wivu marehemu kutangulia mbele za haki.

Post a Comment

 
Top