Menu
 

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mh, Philipo Mulugo.

Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wamiliki wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Serikali nchini wametakiwa kujikita na kuanzisha Shule na Vyuo vya Ufundi Stadi ili kukidhi haja ya ongezeko la wanafunzi wanaomaliza Kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano.
 
Aidha wametakiwa kuendana na mipango ya baadaye ambapo Shule na Vyuo vingi vimejikita katika Michepua ya Sanaa na kusahau Michepuo ya Sayansi kutokana na Nchi kuwa na uhitaji wa Walimu na wataalamu wa Sayansi ambapo pia ameongeza kuwa Serikali itawakopesha Wanafunzi watakaosoma Sayansi.
 
Mwito huo ulitolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu na  Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipokuwa akifunga Mkutano wa Mwaka wa Wamiliki, Mameneja na Wakuu wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali (TAMONGSCO) uliofanyika Kitaifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Jijini Mbeya.
 
Alisema Wamiliki wa Vyuo wanaouwezo wa kujenga Shule na Vyuo vingine hivyo wajikite katika Michepuo ya Sayansi ili kuisaidia Serikali katika Kuziba pengo la upungufu wa Wataalamu wa Sayansi ambapo pia aliongeza kuwa Serikali imewapa kipaumbele cha Mikopo wanaochukua michepuo hiyo.
 
Naibu Waziri aliongeza kuwa ili kuondoa migogoro baina ya Serikali na Shule binafsi ni vema kila anayetaka kuanzisha Shule au Chuo  pamoja na Vyuo vilivyopo ambavyo havijajiunga na Umoja wao kufanya hivyo mara moja, lakini ambaye hatajiunga na umoja huo hataweza kupata ufafanuzi wa maswala yoyote anayoyahitaji kutoka Serikalini.
 
Mulugo alisema Wenye mashule na vyuo binafsi wengi hawana uelewa juu ya Wizara ya Elimu, Tamisemi  na ngazi zinazohusika na Elimu hivyo njia rahisi ya kuwaelimisha ni kupitia umoja wao ambapo aliongeza kuwa katika kulisisitiza Hilo atahakikisha anamwagiza Kamishna wa Elimu na Nekta kuwasisitiza umuhimu wa kujiunga na umoja.
 
Awali akimkaribisha Naibu Waziri kufunga Mkutano huo Mwenyekiti wa TAMONGSCO Taifa Mahamoud Mlingo alisema umoja wao  unakabiliwa na Changamoto nyingi kutoka Serikalini ambazo zinatishia baadhi ya Shule binafsi kuendelea kujiendesha.
 
Alizitaja baadhi ya Changamoto hizo kuwa ni kutolewa kwa Nyaraka nyingi zinazofikia 20 ambazo zinaeleza namna ya kuongoza Elimu hususani Shule za Taasisi Binafsi ambapo baadhi ya Vipengele ndani ya Nyaraka hizo zinapingana na Haki ya Mtanzania ya kupata Elimu Bora kwa njia ya Mchujo.
 
Aliongeza kuwa Mfumo mzima wa kuangalia Viwango vya Ufaulu tangu Mwanzo bila kuwashirikisha Wakuu wa Vyuo na Shule binafsi ndiyo unaochangia Elimu kuendelea kudorora kutokana na Serikali kutothamini mchango unaotolewa na Sekta Binafsi hususani kwenye Elimu ili hali Sekta zingine binafsi zinashirikishwa kutokana na Sera ya PPP.
 
Pia aliongeza kuwa Kushirikiana na Serikali namna ya ya kushirikiana katika Matumizi ya Vyumba vya Madarasa  500 ambavyo viko tupu nchi nzima kutokana na upungufu wa Wanafunzi katika Shule binafsi.
 
Mwenyekiti huyo alisema Changamoto nyingine inayoikabili Sekta binafsi katika Suala la Elimu ni gharama kubwa za uendeshaji kutokana na kuchangia michango mingi Serikalini kama Zimamoto na Osha pamoja na Kodi za kawaida ili hali huduma ya Elimu ni huduma ya Jamii ambayo haipaswi kuwa na michango mingi.
 
Aliitaja Changamoto nyingine kuwa ni Serikali kupokonya Wanafunzi wote kutokana na ujenzi wa Shule za Kata ambapo Shule binafsi hukosa wanafunzi hivyo kupelekea Shule hizo kushindwa kujiendesha kutokana na kuwa na wanafunzi wachache.
 
Akijibu baadhi ya Changamoto hizo Naibu Waziri Mulugo alisema ni vema wakaandika madai yao yote ili yakaye kwenye maandishi ili Serikali ianze kuyafanyia kazi moja baada ya jingine  ambapo alisema pia kuna kamati maalumu imeundwa ili kuyafanyia kazi madai ya baadhi ya Vyuo n Shule binafsi kutoza ada kubwa inayowaumiza wazazi.
 
Pia aliongeza kuwa Serikali imeanza kuyafanyia kazi baadhi ya mambo ikiwemo Maswala ya Sheria ambazo zilitungwa muda mrefu na haziendani na mfumo wa sasa wa uendeshaji wa Elimu.

Post a Comment

 
Top