Menu
   Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leodger Chilla Tenga 
 =====
 
Na Shaban Kondo.
Shirikisho la soka nchini TFF, linajipanga kuwawandikia barua baadhi ya viongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans waliotoa taarifa za kuhisi timu yao inahujumiwa kufuatia mabadiliko ya ratiba la ligi kuu yaliyofanywa na kuepeleka mchezo wao dhidi ya Oljoro JKT kusogezwa mbele kutoka siku ya jumatano hadi siku ya jumamosi.

Katibu mkuu wa TFF Angetille Osiah amesema viongozi hao wataandikiwa barua ya kuwataka wajieleze kwa kina juu ya suala la hujuma wanahisi kufanyiwa na endapo watashindwa kufanya hivyo suala hilo litapelekwa kwenye kamati ya nidhamu kwa ajili ya kujadiliwa.

Katika hatua nyingine Angetille Osiah amewataka viongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans kuacha uoga na kutambua soka siku zote linachezwa uwanjani na hakuna sehemu nyingine ya kusaka point tatu, hivyo inawalazimu kuacha visingizio visivyokua na maana kwa wadau wa soka nchini kote.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya simba umeshangazwa na kauli iliyotolewa na viongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans ya kutotambua mpango wa kuonyeshwa moja kwa moja kwa baadhi ya michezo ya mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema suala la michezo hiyo kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sports lilizungumzwa katika mkutano wa uongozi wa kituo hicho na vilabu vya ligi kuu uliofanyika kwenye hoteli ya Southern Sand.

Post a Comment

 
Top