Menu
 


Mbu wanaoambukiza Malaria huvutiwa zaidi na harufu ya mwili wa binadamu kuliko wadudu wengine, kwa mujibu wa utafiti.

Watafiti waliochapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la Plos One, wanaamini kuwa Mbu wanaobeba viini vinavyosababisha Malaria, huwa na uwezo mkubwa wa kunusa.

Daktari James Logan, kutoka chuo cha mafunzo ya fya mjini London, anasema kuwa moja ya mambo ambayo humshangaza ni ambavyo viini vinakuwa na akili nyingi.

Anasema kuwa viini vinaonekana kuwa na akili nyingi kiasi cha kuwa mbele kwa fikira kuliko hata wanasayansi.

Miguu yenye kunuka

Katika kufanya utafiti wao, wanasayanyi waliwaambukiza Mmbu na viini hatari vya Plasmodium falciparum.

Waliwaweka Mmbu hao katika mkebe pamoja na soksi ilyoikuwa inavunda na ambayo ilikuwa imevaliwa kwa masaa ishirini. Mmbu hao walijazana kwenye soksi hiyo

Wanasayansi hao walifanya utafiti huo na Mmbu ambao walikuwa hawana viini hivyo.

Waligundua kuwa Mmbu waliokuwa na viini waliweza kuvutiwa zaidi na soski zilizokuwa na uvundo.

Wanasayansi wanaamini kuwa Mmbu waliokuwa na viini wanakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kunusa kwa sababu viini ndivyo vinawawezesha kunusa zaidi.

Kwa Mmbu, binadamu anakuwa rahisi kushambulia kwa sababu ya harufu ya mwili wake na kisha viini hivyo ninavamia damu yake kuhakikisha kuwa vinaendelea kuzaana.

Watafiti hao sasa watafanya utafiti wa miaka mitatu kutaka kujua ni vipi viini vina uwezo wa kufanya hivyo.

Daktari Logan , anasema kuwa ikiwa wataweza kujua viini vinavyosababisha Malaria, itawasaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni, shirika la afya duniani linasema kuwa mnamo mwaka 2012, takriban watu milioni 219 waliugua Malaria huku wengine 660,000 wakiripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Afrika ndilo bara lenye visa vingi vya watu kuugua Malaria na asilimia tisini ya vifo vinavyotokana na Malaria hutokea barani humo.

Post a Comment

 
Top