Menu
 


Kituo cha Bomba Fm 104.OMHz Mbeya kimetangaza ajira moja katika kituo hicho, ambapo mmoja kati ya watu watakaokuwa wakiwania nafasi hiyo ya ajira watashindana moja kwa moja kupitia vipindi viwili.
 
Mshindi wa mashindano atapatikana kwa ushirikiano mkubwa kati yake na wasilikilizaji ambao ndio watakuwa majaji wakuu……

VIGEZO vya mshiriki:-
1. Awe na umri wa kuanzia miaka 18.
2. Awe raia wa Tanzania.
3. Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha nne.
4. Awe hana mkataba wowote na kampuni yoyote ile.
5. Awe hajawahi kufungwa jela au kushitakiwa na kosa lolote.
6. Awe na akili timamu.

*Mwisho wa uchukuaji Fomu ni June 15, 2013.

*Fomu ya ushiriki ni shilingi 10,000/= tu ya Kitanzania   

*Kama upo nje ya Mkoa wa Mbeya maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia simu ya mkononi.+255764 240 440 na vilevile unaweza kulipia gharama ya Fomu kupitia namba hiyo hiyo.

Post a Comment

 
Top