Menu
 


RAISI  JAKAYA KIKWETE AKIPOKEA MAANDAMANO YA WATUMISHI WA PSPF KATIKA UWANJA WA SOKOINE JIJINI MBEYA


MOJA YA WATUMISHI WA PSPF  AKITOA MAELEZO MAFUPI KWA MOJA YA WATEJA WAO


MTUMISHI AKIKABIDHIWA KIPEPERUSHI

WANANCHI MBALIMBALI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WALIPITA KATIKA BANDA HILO LA PSPF KUJUA JINSI SHILIKA HILO LINAVYOFANYA KAZIPicha na Ezekiel Kamanga & Mbeya Yetu Blog
MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) ulioanzishwa Mwaka 1999 kutokana na Sheria ya Bunge kifungu namba 2 ya Mwaka 1999 inajivunia kuwa mfuko unaoongoza kwa kulipa mafao bora kwa watumishi.

Wakizungumza na Mwandishi wetu wakati wa kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya ambao hawakutaka majina yao yaandikwe kutokana na maadili ya kazi yao walisema miongoni mwa mashirika yanayotoa mafao Nchini PSPF ndilo shirika bora kuliko yote.

Walisema  ubora wa Shirika lao unatokana na mtindo wa kulipa mafao kwa wanachama wake wastaa kwa kutumia mshahara wa mwisho wa mfanyakazi tofauti na mashirika mengine yanayoangalia mishahara ya miezi sita.

Walisema shirika lao linajivunia mafanikio mengi ikiwemo ya uwekezaji uliosalama ambapo fedha za mwanachama hufanyiwa miradi ikiwemo kumkopesha mwanachama anayekaribia kustaafu kutokana na wafanyakazi wengi kukosa mahali pa kuishi baada ya kustaafu.

Waliongeza kuwa fedha zinazotolewa na shirika lao zinathamani kubwa ambapo hadi kufikia Mwezi Machi Mwaka huu Shirika lina thamani ya Shilingi Trilion 1.2 kutoka kwa wanachama zaidi ya 340,000.
Walifafanua zaidi kuwa Shirika hilo limeanzisha mpango wa uchangiaji wa hiari kwa watumishi wasio na ajira maalumu ambapo mafao yao yatakuwa kwenye Elimu, Ujasiliamali, Ugonjwa mirathi, mirathi na kujitoa kazini.

Pia walisema shirika hilo limeanzisha mradi wa ujenzi wa nyumba kwa wanachama ambao ni wamuda wa miaka mitano na kuendelea ambapo tayari mikoa mitano imeanza kunufaika ambayo ni Dar Es Salaam, Mtwara, Tabora, Morogoro na Shinyanga huku ujenzi ukitarajiwa kuanza katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Iringa na Kilimanjaro ambako viwanja vimepatikana tayari.

Post a Comment

 
Top