Menu
 

SHULE ya msingi ya Idugumbi iliyopo Mbeya vijijini, 
Mwalimu Mkuu wa shule ya Idugumbi Mpaze Mchaba, amesema licha ya shule hiyo kuwa na madarasa ya kutosha , madawati pamoja na walimu lakini watoto waliopo ni 270.
Akizungumzia tatizo hilo Mtendaji wa kijiji cha Idugumbi Deodath Msyaliha, amekiri kuwepo kwa utoro wa wanafunzi pamoja na wazazi kuwatumia watoto kwenye shughuli hizo za uzalishaji kwa kutumia kilimo cha kahawa.
Wanafunzi wachache waliofika shuleni
Baadhi ya wazazi walioitwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo wakimsikiliza mwalimu huyu juu ya watoto wao kutofika shule
“Baada ya kubaini tatizo hili tulilifikisha kwenye serikali ya kijiji na kuazimia kuwa kila mtoto atakaye toroka shule mzazi atawajibika kutoa shilingi 2000 kila siku atakaye kosa masomo tukiamini wazazi watajirekebisha na kuwahimiza watoto kufika shuleni  hali ambayo ni tofauti,”alisema
Shule ya msingi ya Idugumbi iliyopo Mbeya vijijini, inakabiliwa na uhaba wa wanafunzi kutokana na wazazi kuwatumia watoto hao kwenye shughuli za uvunaji wa zao la kahawa.

Akizungumzia tatizo hilo, Mwalimu Mkuu wa shule ya Idugumbi Mpaze Mchaba, alisema licha ya shule hiyo kuwa na madarasa ya kutosha , madawati pamoja na walimu lakini watoto waliopo ni 270.

Alisema, uhitaji wa shule ni watoto zaidi ya 400 lakini mpaka sasa ni watoto 270 ndio wanaohudhuria masomo darasani na kati yao ni watoro wa kudumu.

Alisema, kamati ya shule ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatumikisha watoto kwenye shughuli ya kilimo kama vile kuvuna kahawa na kupeleka viwandani.

“Baada ya kubaini tatizo hili tulilifikisha kwenye serikali ya kijiji na kuazimia kuwa kila mtoto atakaye toroka shule mzazi atawajibika kutoa shilingi 2000 kila siku atakaye kosa masomo tukiamini wazazi watajirekebisha na kuwahimiza watoto kufika shuleni  hali ambayo ni tofauti,”alisema.

Akizungumzia tatizo hilo Mtendaji wa kijiji cha Idugumbi Deodath Msyaliha, amekiri kuwepo kwa utoro wa wanafunzi pamoja na wazazi kuwatumia watoto kwenye shughuli hizo za uzalishaji kwa kutumia kilimo cha kahawa.

Aliwataja baadhi ya wazazi hao kuwa ni Isaya Waziri, Yohana Waziri, Julius waziri na Msuya Waziri ambao wote kwa pamoja walikiri kwa maandishi mbele ya kamati ya shule kuhusika na ukatishaji watoto masomo na kukubali kulipa lakini mpaka sasa hawajatekeleza.

Aidha, Mtendaji huyo, alisema suala hilo limefikishwa kwenye ofisi ya Mtendaji Kata na Diwani ili watuhumiwa hao washughulikiwe kwa kuwakatisha watoto masomo darasani kama taratibu za elimu zinavyoeleza.

Wakati huo huo, Shule ya msingi ya Mbalizi na Mageuzi zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na ukosefu wa matundu ya vyoo.

Akizungumzia hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Mapinduzi Nelsoni Mwakyusa, alisema kijiji kilitoa shilingi 200,000 katika kukamilisha ujenzi wa matundu  24 ya vyoo vipya ambapo matundu ya awali yalititia kutokana na mvua za masika.

Alisema, kutokana na tatizo hilo shule hizo hazitakuwa na likizo katika kufidia muda ambao watoto walikaa nyumbani na kukosa masomo kwa zaidi ya miezi miwili.
Picha na Ezekiel . Kamanga

Post a Comment

 
Top